Home Sports YANGA WASIMIKA MNARA MWINGINE HUKU

YANGA WASIMIKA MNARA MWINGINE HUKU

MABINGWA watetezi wa Kombe la Azam Sports Federation Yanga wamewafungashia virago katika raundi ya pili Hausing FC ya kutoka Njombe katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Dakika 45 za mwanzo mchezo ulikuwa ni wa upande mmoja kwa Yanga kumiliki zaidi na kufunga mabao 4-0 Hausing ambao angalau waliongeza ushindani kipindi cha pili walipofungwa bao moja na kufunga bao moja.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Jonas Mkude dakika ya 19, Skudu Makudubela dakika ya 25 huku Clement Mzize akifunga hat trick dakika ya 27, 33 na 56 huku bao pekee la Hausing FC lilifungwa na Tonny Jailos.

Ni mnara wa 5 G Yanga wamesimika  kwenye mchezo wa leo Uwanja wa Azam Complex huku Mzie akiwa kwenye ubora ndani ya uwanja akitimiza majukumu yake.

Mkude kwenye eneo la kiungo alifanya kazi yake kuwazuia wapinzani wasipeleke mashambulizi kwa Aboutwalib Mshery ambaye hakupata usumbufu mwingi langoni.

Previous articleTajirika na Maokoto ya Meridianbet Leo
Next articleMITAMBO YA KAZI AZAM FC INAPIKWA UPYA