Home International DR CONGO WAIDUWAZA MISRI AFCON

DR CONGO WAIDUWAZA MISRI AFCON

TIMU ya taifa ya DR Congo iliyokuwa kundi F na timu ya taifa ya Tanzania imekata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON).

Ilikuwa katikà 16 bora dhidi ya Misri ya Mohamed Salah ambaye kagotea hatua hiyo na mpango wa kutinga nusu fainali umeyeyuka mazima.

Wababe hao walitinga hatua ya robo fainali baada ga kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 ambapo ni Mustafa Mohamed dakika ya 45 alifunga kwa Misri na Mechak Elia alifunga kwa DR Congo dakika ya 37.

Pia ndani ya DR Congo yupo mshambuliaji Fiston Mayele ambaye naye aliwahi kucheza katika Ligi Kuu ya Tanzania.

Ushindi ulikuwa ni Misri penalti 7-8 DR Congo huku moja ya penalti ikipigwa na Henock Inonga anayecheza Ligi Kuu Bara ya Tanzania.

Pia Guinea ya Ikweta imefungashiwa virago katika 16 bora kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Guinea

Previous articleWATAKUJA KIVINGINE KABISA CAF YANGA
Next articleINGIZO JIPYA SIMBA LIMEPEWA JEZI NGUMU