>

INGIZO JIPYA SIMBA LIMEPEWA JEZI NGUMU

INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Simba limepewa jezi ngumu ambayo ni namba 18 iliyokuwa inavaliwa na kiraka aliyeonja chungu na tamu na uwezo wake ulikuwa mkubwa kwenye kutimiza majukumu yake kila alipopewa nafasi. Michael Fredy ameanza mazoezi na wachezaji wa Simba akiwa ni mshambuliaji anayetarajiwa kubeba mikoba ya Jean Baleke ambaye amekutana na Thank You.