Home Uncategorized VISA ZAIDI YA 10 KWENYE GANZI YA MAUMIVU VILITOKEA

VISA ZAIDI YA 10 KWENYE GANZI YA MAUMIVU VILITOKEA

IKUFIKIE popote ulipo kwamba kwenye simulizi ya Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo iliyokuwa ikiandikwa ndani ya Championi Jumatano kuna visa zaidi ya 10 ambavyo vilitokea katika maisha ya kila siku.

Ikumbukwe kwamba simulizi ya Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo inaingia kwenye orodha ya simulizi bora zilizopata nafasi ya kuchapishwa ndani ya gazeti la Championi Jumatano ni utunzi wa Lunyamadzo Mlyuka.

Kwa sasa mchakato unaendelea kufanyia kazi maombi ya wasomaji ipatikane kwenye kitabu kinachotarajiwa kutoka hivi karibu na oda kutoka sehemu mbalimbali zimeanza kutolewa ikiwa ni pamoja na Lindi, Njombe, Kibaha hivyo bado kuna nafasi ya kutoa oda pamoja na udhamini.

Akizungumza kuhusu visa hivyo, mwandishi Mlyuka aliweka wazi kuwa alipata kushuhudia matukio zaidi ya 10 kwenye jamii na kuyafanyia kazi kwa kuyaweka kwenye maandishi kufikisha ujumbe kwa jamii.

“Kuna matukio zaidi ya 10 ambayo ni visa vya ukweli moja ya hayo ni tukio lililotokea kwenye barabara kuu ya magari ambapo mjasiriamali alipigwa na ganzi asijue la kufanya na ndoo aliyobebea maandazi ilidondoka. Ilikuwa ni huzuni kwa kuwa wengi walidhani labda angepata ajali mwisho alipona.

“Mbali na hilo pia kuna sekeseke la wanafunzi kufukuzwa shule kutokana na ada, kuachwa njia panda katika mahusiano hivi ni baadhi ya visa ambavyo vipo katika simulizi ya Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, ni muda wa kusubiri kupata kitabu,”.

Kwa oda, udhamini wasiliana moja kwa moja na mwandishi 0756 028 371. Kwa sasa simulizi inayoendelea ni Msichana wa Maisha Yangu, ndani ya Championi Jumatano.

Previous articleVUNA MAPESA YA KASINO| CHEZA THE MONEY MEN MEGAWAYS
Next articleBETPAWA YANOGESHA AFCON KWA KUTOA ZAWADI