>

AZAM FC HAWAPOI

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Yusuph Dabo amesema kuwa kikubwa ambacho wachezaji wake wanatakiwa kukifanya ikiwa ni pamoja na kiungo Feisal Salum, mshambuliaji Prince Dube ni kujitoa muda wote kutafuta ushindi.

Timu hiyo maskani yake ni Dar inatumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi zake za nyumbani. Kwenye ligi baada ya kucheza mechi mbili ni pointi sita zipo kibindoni.

Dabo ni shuhuda wa nyota Feisal kuwa wa kwanza kufunga hat trick ndani ya kikosi cha Azam FC katika mchezo dhidi ya Tabora United.

Kocha huyo amesema: “Kwa namna ambavyo tunafanya maadalizi kwa mechi zijazo ni muhimu kwa wachezaji kucheza kwa kujitoa zaidi ili kupata matokeo mazuri uwanjani.

“Tunaamini kuna makosa ambayo yanatokea hayo tunayafanyia kazi ili kuwa imara kwa mechi zijazo. Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazo nasi tunajitahidi kufanya kazi nzuri kupata matokeo,”.

Mchezo ujao kwenye ligi kwa Azam FC unatarajiwa kuwa dhidi ya Singida Fountain Gate ambao utapangiwa tarehe.