Home Sports MUDA NI SHUJAA WA GAMONDI

MUDA NI SHUJAA WA GAMONDI

KIUNGO mzawa Mudathir Yahya anayekipiga ndani ya Yanga ni shujaa chini ya Miguel Gamondi kutokana na uwezo wake kila anapopata nafasi.

Nyota huyo kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alionyesha mekeke yake alipotokea benchi.

Baada ya dakika 90 kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa ubao ulisoma Yanga 1-0 Namungo FC na mtupiaji alikuwa Mudhathir.

Bao hilo la kwanza lilipachikwa dakika ya 87 ikiwa imebaki dakika chache mchezo kugota mwisho.

Ushindi huo unaipa Yanga pointi tatu wakiwa namba moja kwenye ligi na pointi zao kibindoni ni 9 baada ya kucheza mechi tatu na hawajapoteza mchezo ndani ya ligi.

Previous articleAZAM FC HAWAPOI
Next articleBALEKE JINA LAKE LIMESOMA