Home Sports BALEKE JINA LAKE LIMESOMA

BALEKE JINA LAKE LIMESOMA

JEAN Baleke ni nyota wa pili kufunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja ndani ya Ligi Kuu Bara.

Jina lake limesoma kwenye orodha ya mastaa wenye hat trick Bongo ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Septemba 21 ubao ulisoma Simba 3-0 Coastal Union na mabao yote yalifungwa na Baleke.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo huo beki wa Simba, Henock Inonga alipata maumivu ya mguu baada ya kuchezewa faulo na nyota wa Coastal Union, Haji Ugando.

Jina la kwanza kusoma kwa nyota wenye hat trick Bongo ni Feisal Salum aliyefunga kwenye mchezo dhidi ya Tabora United uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Baleke alifunga wakati Simba ikikomba pointi tatu dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Uhuru.

Previous articleMUDA NI SHUJAA WA GAMONDI
Next articleVIDEO: AHMED ALYY AFUNGUKIA ISHU YA HENOCK INONGA