>

VIDEO: AHMED ALYY AFUNGUKIA ISHU YA HENOCK INONGA

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa beki wa Simba Henock Inonga hajavunjika baada ya kuchezewa faulo kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union.

Simba inafikisha pointi tisa sawa na Yanga ambao ni vinara wa ligi msimu wa 2023/24.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru ubao ulisoma Simba 3-0 Coastal Union na kukomba pointi tatu kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa