SIMBA WAKUTANA NA KISANGA UGENINI

NGOMA ni nzito kwa Simba kimataifa baada ya kuruhusu mabao mawili sawa na Yale waliyofunga licha ya kupata nafasi zaidi ya tatu.

Ni kisanga kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira raia wa Brazil ambaye alianza kushuhudia wakitunguliwa mapema ugenini.

Mabao yote ya Simba yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 59 na 90 huku Power Dynamo dakika ya 28 kupitia kwa Joshua Mutale na Mulombwa dakika ya 74 akimtungua Ayoub Lakred akiwa nje ya 18.

Huo ni mchezo wa kwanza kwa Ayoub kuanza kikosi cha kwanza baada ya kusajiliwa kwenye usajili wa dirisha kubwa.