SINGIDA FOUNTAIN GATE KWENYE JAMBO LA WATANZANIA

UONGOZI wa Singida Fountain Gate umeweka wazi kuwa mchezo wao wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Future ya Misri unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Azam Complex ni jambo la Watanzania.

Timu hiyo inatupa kete yake saa 10 jioni huku mashabiki wakiombwa kujitokeza kwa wingi kuishangalia timu hiyo inayopeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa.

Hussein Masanza, Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate amesema  wanatambua kazi kubwa ni kusaka ushindi jambo ambalo litafanyika.

“Kwenye jambo la Watanzania hakutakuwa na kiingilio, shabiki aje Uwanja wa Azam Complex akiwa na uzi wa timu yake ataingia kushangilia mchezo wetu hili ni jambo letu sote Watanzania.

“Benchi la ufundi limekamilisha maandalizi yake na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani muhimu kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi,”.