Home International YANGA WATOA BURUDANI KIMATAIFA UGENINI

YANGA WATOA BURUDANI KIMATAIFA UGENINI

BURUDANI imetolewa kwa Wananchi kàtika anga la kimataifa wakishuhudia ubao ukisoma Al Merrick 0-2 Yanga

Chini ya Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamond ukuta umekuwa imara licha ya kutokuwepo kwa nahodha Bakari Mwamnyeto ambaye ana matatizo ya kifamilia.

Kennedy Musonda dakika ya 60 na Clement Mzize dakika ya 79 walikamilisha kazi ya kwanza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Rwanda.

Yanga inakamilisha dakika 90 za awali ikiwa haijafungwa kwenye mchezo wa kimataifa uliokuwa una ushindani mkubwa.

Kete inayofuata kwa Yanga ambayo itawafungulia njia ya kutinga hatua ya makundi inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Previous articleKIMATAIFA: AL MERRIKH 0-0 YANGA
Next articleSINGIDA FOUNTAIN GATE KWENYE JAMBO LA WATANZANIA