Home International ANSU FANTI NDANI YA BRIGHTON

ANSU FANTI NDANI YA BRIGHTON

RASMI sasa mshambuliaji Ansu Fati atavaa jezi
za Brighton baada ya Alhamisi kukamilisha
dili lake la kujiunga na timu hiyo kwa mkopo
akitokea Barcelona.

Fati ametolewa kwa mkopo Brighton baada ya
kushindwa kumshawishi kocha wa Barcelona,
Xavi Hernandez licha ya awali kuonekana kinda

huyo atafanya makubwa kikosini hapo kiasi cha
kukabidhiwa jezi namba 10 iliyovaliwa na staa
mkubwa kikosini hapo, Lionel Messi.

Fati amejiunga na Brighton katika dili ambalo
litadumu hadi Juni 2024 kukiwa hakuna
kipengele cha kununuliwa moja kwa moja na
klabu hiyo ya England.

Previous articleBOSI AANIKA FAILI LA YANGA, SIMBA YATAMBA KUWACHAPA WAARABU
Next articleBOSI SIMBA: AL AHLY NDIO TULIKUWA TUNAWATAKA, YANGA YAVUJISHA SIRI