Home Uncategorized NDONDO CUP YAFIKA 16 BORA

NDONDO CUP YAFIKA 16 BORA

BAADA ya kivumbi kutimka hatua za makundi mashindano ya Ndondo Cup hatimaye 16 bora imepatikana na inatarajiwa kuanza Agosti 12-16 na viwanja viwili vitatumika ikiwa ni Uwanja wa Kinesi na Bandari.

Mashindano hayo yenye ushindani mkubwa yanaratibiwa na Chama cha Soka wilaya ya Ubungo.

Katibu wa chama cha soka wilaya ya Ubungo, Hassan Bakari  amesema:”Kwa sasa zinatafutwa timu nane zitakazotinga  hatua ya robo fainali na 16 bora mashabiki watashuhudia  kwa kiingilio cha shilingi elfu mbili.

“Timu zilizofanikiwa kutinga hatua hiyo ni pamoja na Rajaa FC, Keko Furniture,  Mabibo Market, Kibangu Rangers, Kauzu FC, Temeke Manispaa, Sinza Star, Weekend Team, Uruguay  Fans, Azimio FC, Madenge FC, Bahari FC, Magomeni Combine na Wajerumani FC, “ amesema Bakari.

Previous articleKIPA SIMBA KWENYE MTEGO MKWAKWANI
Next articleHUYU HAPA KIPA MPYA SIMBA