Home Sports KIPA SIMBA KWENYE MTEGO MKWAKWANI

KIPA SIMBA KWENYE MTEGO MKWAKWANI

ALLY Salim kipa namba mbili wa Simba ameingia kwenye mtego mwingine wa kudhihirisha ubora wake kama alibahatisha ama ulikuwa ni upepo alipokamilisha dakika 90 bila kutunguliwa na mastaa wa Yanga wakiongozwa na Fiston Mayele.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 Salim alikaa langoni kwenye Kariakoo Dabi na alishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa mzunguko wa pili ukisoma Simba 2-0 Yanga.

Jitihada za Mayele mzee wa kutetema aliyekamilisha ligi akiwa na mabao 17 akitwaa tuzo ya ufungaji bora alikwama kumtungua Salim kwenye mchezo huo.

Hatimaye ameingia kwenye mtego mwingine ambao unatarajiwa kujibu baada ya dakika 90 Agosti 13 kwenye Kariakoo Dabi itakayopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Yanga v Simba zitamenyana kumsaka mshindi wa Ngao ya Jamii ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya langoni kwa Simba anatarajiwa kukaa Salim kutokana na maumivu aliyonayo kipa namba moja Aishi Manula.

Previous articleMUDA NI MCHACHE HUKU MAMBO YAKIWA MENGI
Next articleNDONDO CUP YAFIKA 16 BORA