Home Sports HUYU HAPA KIPA MPYA SIMBA

HUYU HAPA KIPA MPYA SIMBA

RASMI Simba imemtangaza kipa mpya mwingine tena ambaye atakuwa askihirikiana na wale waliopo kwenye kazi ya ulinzi.

Ni Ayoub Lakred Agosti 12 ametambulishwa rasmi huku taarifa zikieleza kuwa ni Agosti 11 dili lake lilikuwa tayari kwa mwamba huyo kuwa ndani ya Simba.

Kipa huyo alikuwa anaitumikia Klabu ya AS Far ya Morocco hiyo msimu wa 2023/24 atakuwa ndani ya Simba.

Awali Simba ilimtambulisha Luis Jefferssen raia wa Brazil huyu alipata maumivu kambini Uturuki na kufikia makubaliano ya kuachana naye jumlajumla.

Anaungana na Aishi Manula ambaye ni kipa namba moja anayepambania kurejea kwenye ubora wake huku kipa Ally Salim aliyekuwa ni mbadala wa Manula akirejea kwenye nafasi yake ya kuwa kipa namba tatu.

Agosti 13 atakuwa shuhuda Simba ikicheza fainali na watani zake wa jadi Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Simba ilipata ushindi wa penalti 4-2 Singida Fountain Gate kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Agosti 10.

Kwenye mchezo huo dakika 90 zilikamilika ubao ukisoma Simba 0-0 Singida Fountain Gate.

Previous articleNDONDO CUP YAFIKA 16 BORA
Next articleBINGWA WA EPL HUYU HAPA