Home International BINGWA WA EPL HUYU HAPA

BINGWA WA EPL HUYU HAPA

MSIMU wa Ligi Kuu ya England umeanza kutimua vumbi jana Ijumaa, kwa michezo miwili kupigwa ambapo mabingwa watetezi Manchester City walifungua pazia la kampeni ya kutetea taji lao ugenini mbele ya Burnley, huku mabingwa wa Ngao ya Jamii, Arsenal wao wakianzia nyumbani dhidi ya Nottingham Forest.

Tayari joto la matokeo limezidi kuwa kubwa kwa mashabiki na wadaiu mbalimbali, huku kila mmoja akitaka kuona timu yao inapambana kushinda ubingwa huo.

Kabla hata ya kuanza kwa msimu mpya tayari baadhi ya wachambuzi walianza kutoa utabiri wwao kuhusiana na bingwa wa msimu huu. Miongoni mwa tabiri ambazo zimekuwa zikitolewa na kuaminika zaidi ni ile ya ‘Super Computer’ na baadhi ya wachambuzi na hapa Championi Jumamosi, linakuletea utabiri huo.

Super Computer

Hii yenyewe imetabiri kwamba Manchester City watafanikiwa kutetea tena ubingwa wa Ligi Kuu ya England, mbele ya Arsenal na Manchester United licha ya wapinzani wao hao kutumia pesa nyingi kupitia usajili.

Man City imefanikiwa kushinda ubingwa huo mara tano katika kipindi cha misimu sita iliyopita ambapo msimu uliopita walipindua meza mbele ya Arsenal katika wiki ya mwisho ya msimu na kuwa timu ya kwanza kutoka Uingereza kushinda makombe matatu ‘Treble’ tangu Manchester United ilipofanya hivyo mwaka 1999.

Licha ya kumpoteza, Riyad Mahrez na Ilkay Gundogan katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi, bado wanaonekana kuwa na nguvu ya kutetea tena ubingwa wao. Utabiri huo pia umeiweka Arsenal kumaliza kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo kama ilivyokuwa msimu uliopita, huku Liverpool na Manchester United zikihitimisha utabiri wa nne bora.

Huu hapa utabiri wa msimamo wa Premier unaotarajiwa kuwa kuendana na Supercomputer.

1) Manchester City

2) Arsenal

3) Liverpool

4) Manchester United

5) Chelsea

6) Newcastle

7) Tottenham

8) Brighton

9) Aston Villa

10) West Ham

11) Brentford

12) Crystal Palace

13) Fulham

14) Burnley

15) Everton

16) Nottingham Forest

17) Bournemouth

18) Wolves

19) Sheffield United

20) Luton Town

Wachambuzi

Gary Neville na Jamie Carragher

Gary Neville na Jamie Carragher waipa ubingwa Arsenal, Neville anayechambua kwenye kituo cha habari cha Sky Sports, pamoja na Jamie Carragher wametoa maoni yao juu ya mbio za ubingwa kwa msimu ujao, huku timu za Liverpool, Chelsea na Manchester United vikiachwa nyuma.

Neville alisema: “Arsenal wameonyesha nia ya kweli ya kuhitaji ubinga kutokana na usajili ambao wameufanya. Hii inanifanya nione huenda ikawa ndio timu pekee ambayo nadhani inaweza kushinda ubingwa wa ligi.

“Kwangu sioni Man United, Liverpool au Chelsea kama wanaweza kufanya kitu cha ajabu, Arsenal ndio timu pekee ambayo inaweza kuwapa changamoto City kwa wakati huu.

Carragher, alikubaliana na Neville kwamba Arsenal wana nafasi kubwa kutokana na usajili ambao wameufanya kwenye majira ya joto kwa kuwaleta Declan Rice, Kai Havertz na Jurrien Timber.

Micah Richards

Nyota wa zamani wa Manchester City, Micah Richards alikuwa na matumaini makubwa ya Arsenal kubeba ubingwa lakini majeraha ya straika wao, Gabriel Jesus yamempa wasiwasi ambapo aliiambia BBC: “Nilikuwa karibu kuichagua Arsenal kushinda taji msimu huu, kwa sababu hakuna timu iliyowahi kulitwaa kwa miaka minne mfululizo. Lakini, hawana Gabriel Jesus mwanzoni mwa msimu na nadhani hiyo itawaua tu.”

Michael Owen

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Real Madrid, na Manchester United Michael Owen, ambaye alishinda taji hilo msimu wa 2010-11, naye ametoa utabiri wake ambapo kama ambavyo wengi wametabiri ameipa ubingwa Manchester City.

Katika kukamilisha nne bora, Owen ametabiri ubora wa usajili utawasaidia kufanya vizuri, Manchester United na Liverpool zikikamilisha hesabu ya nne bora.

Previous articleHUYU HAPA KIPA MPYA SIMBA
Next articleLAZIMA TUWAPASUE INONGA, MOLOKO WAREJEA