Home Uncategorized KIUNGO MNIGERIA YAMEMKUTA SIMBA

KIUNGO MNIGERIA YAMEMKUTA SIMBA

VICTOR Ackpan kiungo wa Simba amepewa mkono wa kwa kheri ndani ya kikosi cha Simba.

Kiungo huyo raia wa Nigeria yamemkuta masuala ya ‘Thank You’ kama iliyokuwa kwa Augustino Okra raia wa Ghana.

Kiungo huyo aliibuka ndani ya Simba akitokea kikosi cha Coastal Union ya pale Tanga inayotumia Uwanja wa Mkwakwani kwa mechi za nyumbani.

Ni miongoni mwa nyota waliocheza fainali ya Azam Sports Federation wakati huo alipokuwa ndani ya Coastal Union dhidi ya Yanga.

Alikuwa shuhuda Yanga ikitwaa ubingwa huo kwa ushindi wa penalti baada ya kufungana 3-3.

Hakuwa na msimu bora ndani ya kikosi kutokana na kutokuwa fiti baada ya kujiunga na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira.

Kutokana na kushindwa kupenya kikosi cha kwanza alipelekwa Ihefu kwa mkopo nako mambo yakawa magumu mpaka leo Juni 20 alipopewa mkono wa asante.

Previous articleJULIO ATEMBEZA MKWARA WA MAANA
Next articleYANGA YAFUNGUKIA OFA YA MAYELE