Home Sports JULIO ATEMBEZA MKWARA WA MAANA

JULIO ATEMBEZA MKWARA WA MAANA

KOCHA Mkuu wa KMC Jamhuri Khiwelo, ‘Julio’ amesema kuwa hana hofu na timu yoyote anafanya kazi kubwa kusuka kikosi kwa ajili ya msimu mpya.

Julio amewahi kuifundisha Simba iliyogotea nafasi ya pili kwenye msimamo na aliwahi kuingoza timu hiyo kwenye mchezo wa dabi dhidi ya Yanga.

Yanga ni mabingwa wa ligi msimu wa 2022/23 wamekusanya pointi 78 kibindoni na mtupiaji namba moja kwa Yanga ni Fiston Mayele mwenye mabao 17.

Timu hiyo imejihakikishia nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa PlayOff.

Julio amesema kuwa hakuna timu kubwa bali kuna timu kongwe anatambua namna ya kuzikabili.

“Tumebaki ndani ya ligi kutokana na wachezaji kupambana kwenye mechi za ambazo tumecheza na bado tunaendelea kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya.

“Hakuna timu kubwa kwetu zaidi ni timu kongwe na hizi ninatambua mbinu zao sina mashaka nao tukikutana nao kikubwa kwetu ni kupata pointi tatu ni suala la kusubiri,” amesema.

Previous articleVIDEO:JEMBE AWAVAA VIONGOZI YANGA/MAYELE,DIARRA,BANGALA KUONDOKA
Next articleKIUNGO MNIGERIA YAMEMKUTA SIMBA