Home Sports KIUNGO WA KAZI SIMBA AVUNJA REKODI YAKE

KIUNGO WA KAZI SIMBA AVUNJA REKODI YAKE

MSENEGAL Pape Sakho anayekipiga ndani ya kikosi cha Simba amevunja rekodi yake aliyoiandika yeye mwenyewe msimu wa 2021/22 kwenye suala la kutupia mabao.

Nyota huyo msimu huo alitupia mabao sita kimiani baada ya kucheza jumla ya mechi 22 akitumia dakika 1,355 alitengeneza pasi tano za mabao.

Ikumbukwe kwamba kinara wa utupiaji wa mabao ni Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 16 kibindoni.

Mayele wa Yanga pia msimu wa 2021/22 alitupia mabao 16 hivyo kafikia idadi ya mabao ambayo alifunga msimu uliopita.

Sakho yeye msimu uliopita mabao hayo sita ni matano alitumia mguu wa kulia huku bao moja alitumia mguu wa kushoto na yote alifunga akiwa ndani ya 18.

Msimu wa 2022/23 ni mabao 9 katupia akiwa amecheza mechi 23 akisepa na dakika 1,604 akitumia mguu wa kulia kufunga mabao yote na pasi ya bao katoa moja.

Sakho katupia mabao manne akiwa nje ya 18 na mabao matano akiwa ndani ya 18 hivyo kahusika kwenye jumla ya mabao 10 yaliyofungwa na timu hiyo kati ya 66 yaliyofungwa na Simba.

Licha ya kutupia mabao hayo mengi Simba imegotea nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 baada ya kucheza mechi 28 mabingwa ni Yanga wenye pointi 74.

Previous articleHALLA CITY YAWAVUA UBINGWA REAL MADRID
Next articleAZIZ KI AFICHUA SIRI YA MABAO YAKE