Home International HALLA CITY YAWAVUA UBINGWA REAL MADRID

HALLA CITY YAWAVUA UBINGWA REAL MADRID

MANCHESTER City imetinga hatua ya Fainali ya UEFA Champions League 2022/23 itamenyana na Inter Milan hatua ya fainali.

Real Madrid ambao walikuwa ni mabingwa watetezi wamevuliwa taji hilo rasmi ugenini.

Chini ya Pep Guardiola katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya pili uliochezwa Uwanja wa Etihad iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Ni Bernardo Silva dakika ya 23 na 37 huku Manuel Akanji dakika ya 76 na Julian Alvarez dakika ya 90+1 walipeleka maumivu kwa Real Madrid.

Jumla City imeshinda mabao 5-1 kwa kuwa mchezo wa kwanza ngoma ilikuwa 1-1.

Previous articleYANGA SALUTI
Next articleKIUNGO WA KAZI SIMBA AVUNJA REKODI YAKE