Home Sports AZIZ KI AFICHUA SIRI YA MABAO YAKE

AZIZ KI AFICHUA SIRI YA MABAO YAKE

AZIZ Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga amefichua kuwa mabao yake anayofunga ni kwa ajili ya kutimiza majukumu yake ndani ya timu hiyo kwenye kila mchezo ambao atapata nafasi ya kucheza.

Nyota huyo katupia mabao 9 kibindoni akiwa na pasi tano za mabao baada ya kucheza jumla ya mechi 23 ndani ya msimu wa 2022/23.

Ni msimu wake wa kwanza ndani ya Yanga amehusika kwenye mabao 14 kati ya 56 ambayo yamefungwa na timu hiyo iliyotwaa ubingwa wa ligi ikiwa na pointi 74.

 Aziz KI ambaye miongoni mwa mabao yaliyowaachia lawama makipa ni pamoja na Benedict Haule wa Singida Big Stars pamoja na Aishi Manula wa Simba alisema hiyo ni kazi yake.

“Ninafunga kwa kuwa ninatimiza majukumu yangu na tunashirikiana kuona kwamba tunapata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza kikubwa ni kuona tunafikia malengo ambayo tumepanga.

“Ninafurahi kuwa hapa na ninapenda namna ambavyo tunashirikiana kikubwa ni kuona kazi inaendelea kwani kila kitu ili kikamilike lazima kuwe na ushirikiano na ushindani ni mkubwa,” alisema Aziz KI.

Previous articleKIUNGO WA KAZI SIMBA AVUNJA REKODI YAKE
Next articleYANGA NDANI YA ARDHI YA DAR,KUKIPIGA FAINALI CAF