Home Uncategorized YANGA NDANI YA ARDHI YA DAR,KUKIPIGA FAINALI CAF

YANGA NDANI YA ARDHI YA DAR,KUKIPIGA FAINALI CAF

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga za kimataifa Yanga Mei 19 wamewasili salama kwenye ardhi ya Tanzania.

Msafara wa Yanga ambao umepita kwenye njia ngumu kusaka mafanikio umewasili ukitokea Afrika Kusini ulipokuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Gallants Marumo.

Ni hatua ya fainali imetinga ikiwa na ushindi wa jumla ya mabao 4-1 hatua kubwa ambayo imefanywa kwa kuifunga Galllants nje ndani.

Mchezo wao ujao ni fainali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika unaotarajiwa kuchezwa Mei 28,2023 Uwanja wa Mkapa.

Ni Yanga dhidi ya USM Alger mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi akiweka wazi kuwa wapo tayari.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamewasili salama Bongo ni Kibwana Shomari, Dickson Job, Djigui Diarra, Clement Mzize, Bakari Mwamnyeto na Fiston Mayele.

Previous articleAZIZ KI AFICHUA SIRI YA MABAO YAKE
Next articleSIMBA INA KAZI KUBWA KUBORESHA KILA IDARA