Home Uncategorized SIMBA INA KAZI KUBWA KUBORESHA KILA IDARA

SIMBA INA KAZI KUBWA KUBORESHA KILA IDARA

KWA msimu wa 2022/23 Simba imefeli kwenye kila kitu lakini wachezaji wake wamefaulu kwenye kutengeneza namba nzuri ambazo hazijawa msaada kwa Simba.

Ipo wazi kuwa mchezaji mmoja anashinda mchezo na timu inashinda taji imekuwa hivyo kwa Yanga ambao wameshinda taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Simba imegotea nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 na Yanga ni vinara wakiwa na pointi 74 kibindoni.

Wakati Yanga wakiwa na kinara mmoja kwenye utupiaji ambaye ni Fiston Mayele mwenye mabao 16, Simba wanaye Moses Phiri, Saido Ntibanzokiza hawa wametupia mabao 10 kila mmoja.

2023 mchezaji namba moja kwa kufunga mabao mengi ndani ya ligi ni Jean Baleke akiwa amefunga mabao nane rekodi bora kwa mchezaji ila haijawa na nguvu kwa Simba kupeta.

Kazi kubwa msimu ujao mbali na kuboresha kikosi ni muhimu kwa uongozi kuboresha utendaji wa kazi kwa timu na sio mchezaji mmoja.

Limekuwa likiwapa tabu kwenye kusaka ushindi ikiwa atakosekana mchezaji mmoja kwenye eneo lolote pengo lake linaonekana.

Aishi Manula ambaye ni kipa namba moja alipopata maumivu kila kitu kilibadika kwenye upande wa ulinzi na mikoba yake ikawa mikononi mwa Ally Salim.

Alianza vizuri lakini mwisho ukawa ni mbaya kwa Simba kuondolewa kwenye mashindano yote haina maana kwamba sio kipa mzuri bali tayari wakati anaingia kikosi cha kwanza presha ya kusaka ushindi ilikuwa kubwa kwa kila mchezaji.

Kumbuka mchezaji anashinda mchezo na timu inashinda ubingwa…

Imeandikwa na Dizo Click.

Previous articleYANGA NDANI YA ARDHI YA DAR,KUKIPIGA FAINALI CAF
Next articleYANGA: NINI MWARABU? TUNALITAKA KOMBE, BALEKE AFUNGUKA