
AZAM FC YAIUA KIUME SIMBA NUSU FAINALI
AZAM FC imewaua kiume Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Kombe la Azam Sports Federation mchezo uliochezwa Uwanja wa Nangwada Sijaona. Ubao umesoma Azam FC 2-1 Simba na kufungashiwa virago mazima kwenye mashindano haya mpaka wakati ujao tena. Ni Lusajo Mwaikenda dakika ya 22 alianza kupachika bao kwa Azam FC kisha usawa ukawekwa…