Home Sports MUZIKI HUU WA SIMBA KUWAVAA AZAM FC

MUZIKI HUU WA SIMBA KUWAVAA AZAM FC

BENCHI la ufundi la Simba limebainisha kuwa mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Azam FC watacheza wachezaji wote wa timu hiyo kwa kuwa wanatambua wajibu ni lazima utimizwe.

Ni Yanga wenye taji hilo mkononi ambapo watacheza na Singida Big Stars hatua ya nusu fainali ya pili na mshindi atavaana na atakayepenya leo.

Leo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira inatarajiwa kumenyana na Azam FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Azam Sports Federation, Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Namungo ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na mtupiaji alikuwa Jean Baleke ambaye anafikisha bao lake la 8 kwenye ligi na katika mazoezi ya mwisho miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi ni Clatous Chama, Sadio Ntibanzokiza,Mohamed Hussein, Shomari Kapombe,Joash Onyango na Pape Sakho.

Juma Mgunda, kocha msaidizi wa Simba alisema kuwa ratiba ilikuwa wazi kwa kila mchezaji kuhusu mchezo wao dhidi ya Azam FC hivyo wachezaji wote wapo tayari kuikabili Azam FC.

“Ni mchezo ambao upo kwenye ratiba na wachezaji wanatambua umuhimu wa kupata ushindi kwenye mchezo huo hivyo maandalizi kuhusu mchezo huo yote yamekamilika na mchezaji atakayepangwa anajua atavaa gwanda kuipambania timu.

“Wale wote ambao wamesajiliwa ndani ya Simba ni lazima wacheze na watimize wajibu wao, wapinzani tunawaheshimu kwani sio timu mbaya kufika hatua hii ya nusu fainali tunaamini itakuwa kazi kubwa,”.

Previous articleAZAM FC YAFUNGA KAZI KUIKABILI SIMBA
Next articleWAPINZANI WA YANGA KUTUA BONGO