Home International WAPINZANI WA YANGA KUTUA BONGO

WAPINZANI WA YANGA KUTUA BONGO

MARUMO Gallants kutoka Afrika Kusini ambao ni wapinzani wa Yanga kwenye hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika wanatarajiwa kutua Bongo, Mei 8,2023.

Ni Kesho Jumatatu wanatarajiwa kutua Dar tayari kwa mchezo wao wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Dar Mei 10,2023.

Marumo Gallants jana Mei 7 wametoka kupoteza mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Mamelod Sundowns kwa kuchezea kichapo cha mabao 2-0.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka ushindi ili kutinga hatua ya fainali.

Previous articleMUZIKI HUU WA SIMBA KUWAVAA AZAM FC
Next articleVIDEO:MASHABIKI YANGA WAIBUKA UWANJANI MECHI YA SIMBA V AZAM