Home Sports AZAM FC YAFUNGA KAZI KUIKABILI SIMBA

AZAM FC YAFUNGA KAZI KUIKABILI SIMBA

KALI Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa tayari wamefunga hesabu za mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federatino dhidi ya Simba.

Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga ambao wao watacheza na Singida Big Stars mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti.

Leo Azam FC itakuwa kwenye kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Simba na mshindi atatinga hatua ya fainali kumsubiri mshindi kati ya Singida Big Stars dhidi ya Yanga utakaopangiwa tarehe.

Ni Prince Dube na Idris Mbombo hawa ni washambuliaji wa Azam FC wanaopewa nafasi kuanza kikosi cha kwanza kuikabili Simba kwenye mchezo huo unaotarajiwa ukuwa na ushindani mkubwa.

Kwenye mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting, Dube na Mbombo walitoa pasi za mabao huku Ayoub Lyanga yeye akitupia mabao mawili na Abdul Suleiman alitupia bao moja.

Ongala amesema:”Kwa maandalizi ambayo tumefanya kwa mchezo wetu dhidi ya Simba kila kitu kimekamilika hasa kulingana na muda ambao tulipata kwa ajili ya maandalizi yetu.

“Ni mchezo mgumu tunatambua hilo lakini kazi imekamilika na wachezaji wana ari kubwa kwa ajili ya mchezo wetu ambao ni muhimu na tunahitaji kushinda ili kutinga hatua ya fainali,”.

Previous articleMAKIPA BONGO MAKOSA MUHIMU KUFANYIA KAZI
Next articleMUZIKI HUU WA SIMBA KUWAVAA AZAM FC