AZAM FC V SIMBA,ACHA IWE NA REKODI ZAO

    UKIAMINI umesimama muhimu uendelee kupambana ili usianguke itafahamika leo Mei 7, Uwanja wa Nangwanda Sijaona kwenye mchezo wa nusu fainali Azam Sports Federation.

    Timu zote zinaingia uwanjani zikiwa na kazi ya kusepa na ushindi ili kutinga hatua ya fainali unaambiwa acha moto uwake mshindi apatikane.

    Hapa  tunakuletea namna uimara ulivyo kwa wapinzani hawa wawili namna hii:-

    Safari yao ilipoanzia

    Azam FC 9-0 Malimao FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Desemba 9,2022 hatua ya 64 bora.

    Azam FC 4-1 Dodoma Jiji,Uwanja wa Azam Complex Januari 27,2023 Uwanja wa Azam Complex, hatua ya 32 bora.

    Azam FC 2-0 Mapinduzi FC, Uwanja wa Azam

     Complex, hatua ya 16 bora ilikuwa ni Machi 5,2023.

    Azam FC 2-0 Mtibwa Sugar hatua ya robo fainali, Uwanja wa Azam Complex Aprili 3.

    Hawa hapa Simba

    Simba 8-0 Eagle ilikuwa Desemba 10,2022 Uwanja wa Mkapa kwenye hatua ya 64 bora na ni Moses Phiri alifunga hat trick kwenye mchezo huu.

    Simba 1-0 Coastal Union, Uwanja wa Mkapa mtupiaji alikuwa ni Sadio Kanoute akitumia pasi ya Pape Sakho ilikuwa Januari 28,2023 ilikuwa hatua ya 32 bora

    Simba 4-0 African Sports hatua ya 16 bora, Uwanja wa Uhuru ngoma ilipigwa Machi 2 ni Moses Phiri kwenye mchezo huu alitoa pasi mbili za mabao.

    Simba 5-1 Ihefu ilikuwa ni hatua ya robo fainali Uwanja wa Azam Complex nyota Jean Baleke alifunga hat trick kwenye mchezo huu ilikuwa Aprili 7,2023.

    Mabao mengi

    Mechi mbili kwa timu hizi zilishuhudia mabao mengi yakifungwa ikiwa inamaanisha kuwa wote ni wakali kwenye kucheka na nyavu.

    Azam FC waliitungua Malimao mabao 9 yakiwa ni mabao mengi kwenye hatua zote ambazo walipita huku Simba wao wakiwatungua mabao 8-0 Eagle yakiwa ni mabao mengi kwenye hatua ambazo wamecheza.

    Ukuta wote balaa

    Timu zote zinaonekana kuwa imara kwenye ulinzi ambapo hakuna timu iliyofungwa mabao zaidi ya mawili zote zimetunguliwa bao mojamoja katika mechi 4 walizocheza ambazo ni dakika 360.

    Mabao 17 Azam FC wamefunga wana wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 21 huku Simba wakiwa wamefunga jumla ya mabao 18 wakiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 20.

    Kila timu inaonekana kuwa imara kwenye kila idara kwa kuwa kila unapogusa panagusika na kubonyea.

    Wana kisasi chao

    Wababe hawa wana kisasi chao kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi, Azam FC ilishinda bao 1-0 na ule mzunguko wa pili walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

    Azam FC wanauliza sare iliyopita walipataje wapinzani wao na Simba hesabu zao ni kushinda kwenye mchezo huo ili kutinga hatua ya fainali.

    Wametokea Azam Complex

    Timu zote mbili zimetokea Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi zao za hatua ya robo fainali ikiwa ni chimbo linalowakutanisha nusu fainali.

    Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nangwanda, Sijaona mshindi wa mchezo huu anatarajiwa kukutana na mshindi wa mchezo kati ya Singida Big Stars v Yanga ambao utapangiwa tarehe.

    Mkwanja mezani

    Uongozi wa Azam FC umeweka bonasi kwa ajili ya mchezo huu ambapo Abdulakalim Amin, Mtendaji Mkuu wa Azam FC aliliambia Championi kuwa kuna bonasi ambazo huwa zinatolewa kwa timu.

    Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba aliliambia Championi Jumamosi kuwa wachezaji wanajua wanachopata kutokana na mashindano ambayo wanashiriki.

    Previous articleVIDEO:MASHABIKI YANGA WAIBUKA UWANJANI MECHI YA SIMBA V AZAM
    Next articleKIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA AZAM FC