BAADA ya Sadio Mane kumpiga mchezaji mwenzake wa bayern Munich, Leroy Sane wiki iliyopita nyota huyo amepigwa faini ya pauni 250,000, (Sh.724,445,000).
Pia inatajwa kuwa staa huyo raia wa Senegal yupo kwenye hesabu za kuuzwa mwishoni mwa msimu huu.
Mane alimchapa ngumi ya mdomo Sane kwenye chumba cha kubadilishia nguo wiki iliyopita kwa madai kuwa Sane alimkejeli kwa lugha na vitendo vya kibaguzi baada ya mchezo dhidi ya Manchester City.
Sane alionekana akiwa amevimba mdomo wakati Bayern Munich walipoivaa Hoffenheim wikiendi iliyopita na Mane hakuwepo kwenye mchezo huo wa Bundesliga.
Mane amesimamishwa kwa kitendo hicho huku akikatwa mshahara wake wa pauni milioni 17, (sh.49.2) kwa mwaka.
Hii ni faini kubwa kwa Bayern Munich kutolewa katika historia yao.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)