Home Sports AZAM FC HESABU KWA RUVU SHOOTING

AZAM FC HESABU KWA RUVU SHOOTING

AZAM FC hesabu zao kwa sasa ni mchezo ujao dhidi ya Ruvu Shooting ambao unatarajiwa kuchezwa Morogoro.

Katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara, Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kituo kinachofuata ni Aprili 22 ukiwa ni mchezo wa kufunga mwezi kuukaribisa Mei.

Kali Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kupata matokeo mazuri.

“Tunatarajia kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo zinafuata na tuna amini kuwa utakuwa ni mchezo mgumu na ushindani utakuwa mkubwa ambacho tunahitaji ni kupata pointi tatu,”.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 26 vinara ni Yanga wenye pointi 68 kibindoni.

Previous articleMANE APIGWA FAINI NDEFU KWELI BAYERN
Next articleYANGA MAFIA, CHAMA BALEKE KIKAANGONI SIMBA