Home Sports YANGA KUWAFUATA RIVERS UNITED KAMILIKAMILI

YANGA KUWAFUATA RIVERS UNITED KAMILIKAMILI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa hatua a robo fainali dhidi ya Rivers United ambao ni wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Ni mchezo wa hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika baada ya timu hiyo kutinga wakiwa ni vnara wa kundi.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na kikosi kinatarajiwa kuanza safari kesho Aprili 20,2023.

“Kikosi kitaondoka Dar es Salaam kesho alfajiri na shirika la ndege la Ethiopia kuelekea Nigeria kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali Kome la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United.

“Mchezo huo utakachezwa kwenye Jimbo la Akwa Ibom Kusini mwa Nigeria, hautakuwa mchezo mwepesi lakini tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi, “.

Ni Aprili 23, 2023 mchezo huo wa kwanza wa hatua ya robo fainali unatarajiwa kuchezwa na ule wa pili kumpata mshindi wa jumla unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Previous articleMGUNDA: BAHATI YAO, YANGA WANGEKULA ZA KUTOSHA
Next articleMANE APIGWA FAINI NDEFU KWELI BAYERN