Home Uncategorized PAMPA WAZITAKA POINTI ZA MASHUJAA

PAMPA WAZITAKA POINTI ZA MASHUJAA

KOCHA Mkuu wa Pamba, Yusuph Chippo amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Championship dhidi ya Mashujaa FC  unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nyamagana.

Pamba ya Mwanza ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 23 inakutana na Mashujaa iliyo nafasi ya 4 na pointi 41.

Tippo amesema:“Tunamshukuru Mungu tumefanya maandalizi vizuri cha msingi kwetu ni kupambana kupata pointi tatu, mchezo wetu uliopita dhidi ya Kitoyasce ninawashukuru mashabiki walijitokeza kwa wingi.

“Mechi sio moja bado nyingine zinaendelea sita tukicheza nao tutakuwa tumebakiwa na mechi nne hivyo bado tupo kwenye kampeni na mchezo wetu dhidi ya Mashujaa tunaamini tutafanya vizuri.

“Kitayosce FC wao walikuwa wamejipanga kuzuia na walikuwa na kipa mmoja mzuri ambaye alifanya kazi kubwa nina amini Mashujaa watakuwa wamejiandaa kuzuia  lakini bado tuna nafasi na mashabiki wasichoke wajitokeze kwa wingi kutushangilia,” amesema.

Previous articleSIMBA WAIFUNGIA KAZI YANGA, WAWEKA MKWANJA WA MAANA
Next articleVIDEO:HUYU HAPA NAHODHA SIMBA KUHUSU YANGA KWA MKAPA