Home Sports SIMBA WAIFUNGIA KAZI YANGA, WAWEKA MKWANJA WA MAANA

SIMBA WAIFUNGIA KAZI YANGA, WAWEKA MKWANJA WA MAANA

Mabosi wa Simba wameamua kuifungia kazi Yanga inayonolewa na Kocha, Nasreddine Nabi kwani wamesema hawataki chochote zaidi ya ushindi katika Kariakoo Dabi.

Kutokana na jambo hilo tayari wameandaa bonasi ya kutosha ya zaidi ya Sh 300 Mil kwa wachezaji ili kufanikisha ushindi Jumapili.

Katika mchezo huo, Simba wataingia wakiwa na hasira ya kufungwa mara mbili mfululizo walizokutana katika Ngao ya Jamii msimu huu na uliopita.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mabosi hao wa Simba kitu pekee ambacho wanakitaka katika msimu huu ni kuifunga Yanga, hiyo ni baada ya kushindwa kuifunga kwa misimu miwili.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mabosi hao wa Simba, wameweka nguvu hizo za kuwafunga Yanga kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki wao.

Previous articleBEKI HUYU YANGA KUIKOSA DABI KWA MKAPA
Next articlePAMPA WAZITAKA POINTI ZA MASHUJAA