Home Uncategorized AZAM FC WANAWATAKA SIMBA NUSU FAINALI

AZAM FC WANAWATAKA SIMBA NUSU FAINALI

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho inahitaji kucheza na Simba.

Aprli 3 Azam FC ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali inamsubiri mshindi kati ya Simba na Ihefu icheze naye hatua ya nusu fainali.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa waliwaona mashabiki wengi wa Simba na Yanga wakiwa upande wa Mtibwa Sugar hivyo walichokitaka wamekikosa.

“Tumeshinda dhidi ya Mtibwa Sugar daku tumekula sasa tunawataka Simba, tunawaombea washinde dhidi ya Ihefu ili tukutane nao nusu fainali wao walikuwa wapo upande wa Mtibwa basi wamewakosa.

“Hata wakija Ihefu sisi hatuna tatizo kwani wameona namna tulivyocheza vizuri na wachezaji wamejituma kwa juhudi hivyo yoyote yule aje tutakwenda naye sawa,” .

Previous articleKIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA IHEFU FULL MKOKO
Next articleSIMBA 4-0 IHEFU