Home International YANGA KAMILI KUIVAA BAMAKO, AZIZ KI, MAYELE NDANI

YANGA KAMILI KUIVAA BAMAKO, AZIZ KI, MAYELE NDANI

NASREDDINE Nabi Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Real Bamako yapo tayari.
Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho leo Machi 8 2023 dhidi ya Real Bamako mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Nabi amesema kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa mgumu lakini ni muhimu kwao kushinda.

“Ni mchezo muhimu kwetu kupata ushindi na kila timu inahitaji hivyo kutokana na mashindano haya makubwa na yenye ushindani hilo lipo wazi.

“Maandalizi yapo sawa na tuna amini wachezaji watafanya kazi kutimiza majukumu yao hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna kazi itakavyokuwa,”.

Kwenye mazoezi ya mwisho yaliyofanyika Machi 7,2023 miongoni mwa nyota waliokuwa kwenye mazoezi hayo ni pamoja na Aziz KI ambaye alitoa pasi ya bao kwenye mchezo uliopita nchini Mali.

Bao hilo mtupiaji alikuwa ni Fiston Mayele ambaye alifunga akiwa nje kidogo ya 18 naye yupo kwenye orodha ya wachezaji waliokuwa kwenye mazoezi ya mwisho.

Yanga ilishuhudia ubao ukisoma Real Bamako 1-1 Yanga na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Previous articleHIVI NDIVYO NGOMA ILIVYOPIGWA MPAKA ROBO FAINALI
Next articleIHEFU WAKIMBIZA FEBRUARI