Home Sports IHEFU WAKIMBIZA FEBRUARI

IHEFU WAKIMBIZA FEBRUARI

IHEFU yenye maskani yake pale Mbeya imepeta kwa Februari baada ya kusepa na tuzo mbili mazima.

Ni tuzo ya mchezaji bora ambayo ipo mikononi mwa Yacouba Songne ambaye ni mshambuliaji aliyejiunga na timu hiyo akitokea kikosi cha Yanga.

Yacouba amewashinda wachezaji wenzake ambao ni Elias Maguli wa Geita Gold na  Meddie Kagere wa Singida Big Stars.

Yacouba kwenye dakika 97 ambazo ametumia katika mechi mbili amefunga mabao mawili ilikuwa dhidi ya Singida Big Stars na Dodoma Jiji huku akitoa pasi moja ya bao.

Pia ni Malule Omary ambaye ni meneja wa Uwanja wa Highland Estate unaotumiwa na Ihefu kwenye mechi za ushindani alichaguliwa kuwa meneja bora.

Wamepishana na tuzo ya kocha bora ambayo imekwenda mikononi mwa Mecky Maxime wa Kagera Sugar akiwashinda Nasreddine Nabi wa Yanga na Felix Minziro wa Geita Gold.

Previous articleYANGA KAMILI KUIVAA BAMAKO, AZIZ KI, MAYELE NDANI
Next articleNYOTA HAWA WA KAZI KUIKOSA REAL BAMAKO