NYOTA HAWA WA KAZI KUIKOSA REAL BAMAKO

NYOTA wa Yanga, Jesus Moloko kuna hatihati akaukosa mchezo wa leo dhidi ya Real Bamako kutokana na kutokuwa fiti.

Nyota huyo alipata maumivu kwenye mchezo wa Azam Sports Federation dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulikuwa ni wa hatua ya 16 bora.

Moloko ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ambapo kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa alianza kikosi cha kwanza.

Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-1 TP Mazembe na kuwafanya wakusanye pointi tatu mazima kwenye hatua ya makundi ikiwa ipo kundi D.

Mbali na Moloko pia Sure Boy huyu ana matatizo ya kifamilia hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa leo Machi 8.

“Moloko bado hajawa imara ripoti yake ya mazoezi ya mwisho itaamua kama ataanza kikosi cha kwanza ama la lakini ukweli ni kuwa alipata maumivu.

“Wengine ni wale wenye matatizo ya kifamilia lakini tupo tayari kupambana kupata matokeo,”.

Nabi amesema kuwa mazoezi ya mwisho yataamua kama anaweza kuanza ama la kwani hakuwa fiti.