Home International HELLO THIS IS ANFIELD

HELLO THIS IS ANFIELD

LIVERPOOL, ENGLAND - APRIL 20: Anfield Stadium, the home Liverpool Football Club during the coronavirus (Covid-19) pandemic lockdown at Anfield on April 20, 2020 in Liverpool, England. Amid speculation that some coronavirus related cases in Liverpool could be linked to the Champions League match at Anfield on March 11, the mayor of Madrid has said it was a mistake to allow 3,000 Atletico fans to travel to the game. Liverpool F.C. has led the Premier League since the time major sporting events were suspended in mid-March due to the COVID-19 pandemic. (Photo by Christopher Furlong/Getty Images)

THIS is Anfield, kwenye mlango wa kuingilia uwanja wa Anfield unaotumiwa na Liverpool kipo kibango kilichoandikwa maneno hayo.

Hii ni Anfield, wakati Jurgen Klopp anatua Liverpool aliwakataza wachezaji kukigusa mpaka pale watakapochukua kombe kubwa.

Si kitu kidogo, sio neno la kawaida.Aliwahi kuwepo Bill William Shankly, baba wa Liverpool, kabla hajafa aliwaambia siku akifa mwili wake wauchome moto na majivu wayatawanye uwanjani, kutoka goli moja mpaka lingine.

Mwaka 1981 alivyovuta pumzi yake ya mwisho, walio hai wakafanya kama wosia wake ulivyosema.

Bill Shankly aliishi na Liverpool moyoni, akatamani azikwe nayo nafsini vilevile.

Mwili wake ukateketezwa kisha utaishi kwenye nyasi za Anfield mpaka leo na kesho itakapokosa kesho nyingine.

Labda ndio maana wengi wanasema Anfield ni jehanamu ya soka duniani.

Panatisha, Panaogopesha..

Ni ngumu sana kwenda Anfield kisha ukaishi kwa raha kama bestman wa harusi ya tajiri.

Ni eneo hatari kama kukatisha mitaa ya Tandale kibishoo na earphone zenye mziki laini kutoka kwenye simu yako ya gharama nyakati za giza nene.

Ni Anfield ambapo kuna picha ya Leo Messi akishika kiuno chake kwa fadhaa.

Ni Anfield kulipomfanya Arsene Wenger apate mchecheto mpaka kula mueleka kwenye train station.

Kila bora, hupata wasiwasi anapokanyaga Anfield.

Mshindi mara 7 wa tuzo ya Balloon D Or Lionel Messi hajawahi kufunga Anfield.Mfungaji bora wa muda wote wa Man City Sergio Aguero, hajawahi kufunga Anfield.

Ni sehemu inayoogofya mno, juzi kabla ya mechi Eric Ten Hag kocha wa Man United aliulizwa unaizungumziaje Anfield, akajibu kwa kejeli.

Kwa kujiamini alisema, kwake haoni utofauti wowote ule, size ya kiwanja ipo sawa na viwanja vingine, kuna idadi sawa ya marefa na mechi nyingine, mpira ni wa duara.

Mwisho wa mechi, Man United ubao ulikuwa unasoma goli 7 kwa bila.Na hii imekuja nyakati ambazo Liverpool aliingia uwanjani kama timu isiyopewa nafasi kwasababu ya form bora ya Man United.

Katikati ya uwanja Elliot akampoteza Casameiro, Henderson akatawala kama sio yeye wa siku zote.

Ni matokeo ya Anfield yale, ipo roho tofauti kwenye vifua vya wachezaji wao huzaliwa.

Si swala la ubora pekee, hata morali huwa tofauti Anfield.

Hey world, This is Anfield

Previous articleNYOTA HAWA WA KAZI KUIKOSA REAL BAMAKO
Next articleMERIDIANBET YAIADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE HOSPITALI YA SINZA-IWD