Home Uncategorized SIMBA YAINGIA ANGA ZA TP MAZEMBE

SIMBA YAINGIA ANGA ZA TP MAZEMBE

KATIKA kuimarisha safu ya ushambuliaji ndani ya kikosi cha Simba Zemanga Soze anatajwa kuwa katika hesabu za timu hiyo.

Ngoma nzito inatajwa kuwa kwenye dau ambalo linatakiwa ili kupata saini yake.

TP Mazemba anakokipiga Kwa sasa wanatajwa kuhitaji dau refu kumuuza mchezaji huyo.

Kikosi cha Simba kwa sasa kipo Dubai ambapo kimeweka kambi wa ajili ya maandalizi ya mechi zao zijazo.

Kipo chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliviera raia wa Brazil akishirikiana na Juma Mgunda ambaye ni mzawa.

Habari zinaeleza kuwa kocha huyo anahitaji mashambuliaji ambaye ataongeza nguvu kwenye kikosi hicho akishirikiana na nahodha John Bocco pamoja na Moses Phiri ambaye kwa sasa anatibu majeraha.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa watafanya usajili kuimarisha timu hiyo.

“Bado kuna siku zimebaki kwa ajili ya kufanya usajili tukikamilisha mazungumzo tutawaambia mashabiki wasiwe na mashaka,”.

Ni mchezaji mmoja wamemtambulisha Simba ambaye ni Saidi Ntibanzokiza.

Previous articleLILE BEKI LA KAZI YANGA HILI HAPA
Next articleCHUMA HIKI CHA KAZI KINATUA YANGA KUUNGANA NA MAYELE