Home Uncategorized YANGA KAMILI KUIKABILI KMKM

YANGA KAMILI KUIKABILI KMKM

MCHEZO wa kwanza ndani ya 2023 Yanga itashuka Uwanja wa Amaan leo dhidi ya KMKM saa 2:15 usiku.

Ni Katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi 2023 huku kocha msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze akibainisha kwamba wapo tayari kwa ajili ya ushindani.

 Kaze amesema kuwa wanatambua ushindani ambao upo kwenye mashindano hayo kutokana na timu kujipanga.

“Tunatambua kwamba tutakabiliana na upinzani mkubwa na wachezaji ambao tupo nao wanajua kwamba mashabiki wanahitaji ushindi hivyo lazima watapambana kutimiza majukumu yao.

“Ambacho tunaweza kusema kwa sasa kila kitu kipo sawa kuhusu wachezaji ambao tupo nao hatuna mashaka nao kwani uwezo wao ni mkubwa na wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mechi na mazoezi,” amesema Kaze.

Mastaa ambao watakosekana kwenye mchezo wa leo ni pamoja na Fiston Mayele, Aziz KI, Kibwana Shomari, Dickson Job,Tuisila Kisinda huku nyota Yacouba Sogne akitarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji Yanga.

KMKM ipo chini ya Kocha Mkuu, Hemed Morocco ambaye mchezo wake uliopita alipoteza kwa kutunguliwa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars.

Morocco ameweka wazi kuwa watafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Yanga kupata matokeo chanya.

Previous articleMAPINDUZI YAFANYIKE MAPINDUZI YA KWELI
Next article2022 IMEGOTA UKINGONI,2023 IWE YEYE FURAHA