Home Uncategorized MAPINDUZI YAFANYIKE MAPINDUZI YA KWELI

MAPINDUZI YAFANYIKE MAPINDUZI YA KWELI

WAKATI mwingine kwa sasa kwenye Kombe la Mapinduzi 2023 ambapo kila timu shiriki inafanya kazi kubwa kwenye kusaka ushindi.

Hakuna ambaye hapendi kupata matokeo mazuri kwenye mchezo ambao atacheza hivyo kwa sasa ni muhimu kupata ushindi.

Ukweli ni kwamba wachezaji wamepata nafasi kwenye mashindano haya ambayo ni ya heshima na kila mmoja ana kazi ya kuvuja jasho kusaka ushindi.

Imekuwa kawaida kwa baadhi ya timu kupotezea mashindano haya wakiamini kwamba hayawahusu licha ya kwamba wanashiriki.

Basi kinachotakiwa kwa sasa ni kufanya maandalizi mazuri kwenye mechi zote ambazo watacheza ipo hivyo kwa kila mmoja anafanya kazi kubwa kusaka ushindi.

Pia mbali na wachezaji kusaka ushindi ni muhimu kucheza kwa umakini kwenye kutafuta ushindi na kuwalinda wachezaji wengine.

Ni muhimu kufanya kazi kubwa katika kulindana ili kutoumizana kwa kuwa majukumu bado yanaendelea.

Previous articleSIMBA YATAJA SABABU YA KUTUNGULIWA NA MLANDEGE
Next articleYANGA KAMILI KUIKABILI KMKM