Home Uncategorized YANGA YAFUNGA MWAKA NA POINTI TATU ZA MANUNGU

YANGA YAFUNGA MWAKA NA POINTI TATU ZA MANUNGU

 MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Mtibwa Sugar na Yanga uligotea dakika 26 baada ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuwatibulia mipango mapema wapinzani wao.

Ni bao la Aziz KI dakika ya 26 la kipindi cha kwanza limedumu mpaka dakika 90 za mwamuzi kukamilisha mchezo huo.

Pigo la faulo iliyoonekana kutokuwa na hatari ilimduwaza kipa wa Mtibwa Sugar Razack Kimweri ambaye alikutana na mpira nyavuni.

Mtibwa Sugar inayonolewa na Salum Mayanga inafunga mwaka 2022 kinyonge kwa kutunguliwa ikiwa Uwanja wa Manungu.

Nafasi ambazo walitengeneza kipindi cha pili kupitia mapigo ya kona yaliyokuwa yanapigwa na Issa Rashid hayakuwa na faida kwa timu hiyo yenye maskani yake Morogoro.

Yanga inafikisha pointi 50 ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 19 msimu wa 2022/23.

Previous articleWATATU SIMBA WAPENYA KUWANIA ZAWADI YA MWAKA
Next articleHUKU NDIKO AMEIBUKIA FEI TOTO