Home Sports HUKU NDIKO AMEIBUKIA FEI TOTO

HUKU NDIKO AMEIBUKIA FEI TOTO

2023 kiungo wa mpira mwenye mkataba na Yanga mpaka 2024 umemkutia akiwa ndani ya Dubai ambapo amekwenda kwa ajili ya majukumu yake.

Nyota huyo mwenye mabao sita na pasi mbili za mabao amekuwa kwenye mvutano na mabosi wa timu yake kuhusu mkataba wake.

Fei mwenyewe amewaaga mashabiki na kuwashukuru viongozi kwa muda ambao ametumika ndani ya kikosi hicho.

Kwa upande wa viongozi wameweka wazi kuwa bado ni mali ya Yanga na kuna utaratibu wa kuvunja mkataba ambao upo na unatambulika na FIFA hivyo bado ni mali ya Yanga.

Habari zinaeleza kuwa ameibukia ndani ya Dubai kwa ajili ya mapumziko ya muda kisha michongo ikijibu atarejea Bongo.

Timu inayopewa chapuo kuinasa saini ya nyota huyo ni Azam FC.

Previous articleYANGA YAFUNGA MWAKA NA POINTI TATU ZA MANUNGU
Next articleHAPPY NEW YEAR