Home Sports WATATU SIMBA WAPENYA KUWANIA ZAWADI YA MWAKA

WATATU SIMBA WAPENYA KUWANIA ZAWADI YA MWAKA

NYOTA watatu wa kikosi cha Simba wamepenya kwenye hatua ya kuwania tuzo ya mchezaji bora.

Ni tuzo ya kufungia mwaka 2022 ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Atakayesepa na tuzo hiyo atakuwa amefungua zawadi ya kwanza kutoka kwa mashabiki kwa 2023 kutoka kwa mashabiki.

Ni kiungo Clatous Chama ambaye ni bora eneo la kati katika kucheza timu na mtulivu akiwa uwanjani raia huyu wa Zambia.

Pia yupo mshambuliaji John Bocco ambaye ni nahodha wa Simba akiwa ametupia mabao matatu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

Nyota mwingine ni beki Shomari Kapombe ambaye naye alitupia bao kwenye mchezo uliopita dhidi ya Prisons.

Previous articleAZIZ KI AMTUNGUA KIMWERI
Next articleYANGA YAFUNGA MWAKA NA POINTI TATU ZA MANUNGU