Home Uncategorized NAMUNGO YATUMA UJUMBE HUU MSIMBAZI

NAMUNGO YATUMA UJUMBE HUU MSIMBAZI

KOCHA msaidizi wa Namungo, Shadrack sajigwa amebainisha kuwa wachezaji wote wapo kamili kwa ajili ya kuikabili Simba.

Kikosi cha Namungo kimeshatia timu ndani ya Dar ambapo kilifanya maandalizi ya mwisho Ruangwa,Novemba 13 kabla ya kuibukia kwenye jiji la Biashara.

Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye kikosi hicho ni pamoja na Shiza Kichuya ambaye aliwahi kucheza Mtibwa Sugar na Simba kwa mafanikio pia mtupiaji wao namba moja ni Relliats Lusajo mwenye mabao sita.

Nsajigwa amesema:”Tupo tayari kwa ajili ya kuikabili Simba na tunahitaji pointi tatu na hatuna mchezaji majeruhi,”.

Previous articleMTIBWA SUGAR HASIRA ZOTE KWA COASTAL UNION
Next articleKIUNGO WA KAZI MKUDE KUIKOSA NAMUNGO KESHO