KIUNGO Jonas Mkude wa Simba kesha anatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Mkude ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Juma Mgunda anatarajiwa kukosekana kutokana na kutokuwa fiti kiafya.
Simba imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu kesho itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Namungo ambao nao wanazihitaji pia pointi hizo.
Mgunda amesema:”Mkude ni mgonjwa hayupo vizuri kwa sasa pia hata John Bocco yeye alikuwa ni mgonjwa ameanza mazoezi taratibu,”.
Kwenye ligi Mkude katupia bao moja ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Soccer Football - International Friendly - Italy v Turkey - Stadio Renato Dall'Ara, Bologna, Italy - June 4, 2024 Turkey's Abdulkadir Omur shakes hands with Italy's Riccardo Calafiori after the match REUTERS/Daniele Mascolo