Home Uncategorized MABAO SITA YAKUSANYWA KWENYE MECHI TATU

MABAO SITA YAKUSANYWA KWENYE MECHI TATU

MABAO 6 yalikusanywa kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara zilizochezwa Oktoba 4,2022 katika msimu wa 2022/23.

Mchezo uliokusanya mabao mengi ulikuwa ni ule Ruvu Shooting 1-2 Yanga ikiwa ni mabao matatu kwenye mchezo mmoja.

Watupiaji kwenye mchezo huo ni Feisal Salim dakika ya 52 na Bakari Mwamnyeto dakika ya 71 lile la Ruvu Shooting lile la Ruvu Shooting lilifungwa na Rolland Msojo dakika ya 86.

Mchezo mwingine ulikuwa wa Coastal Union 2-0 Kagera Sugar huku mabao yote yakifungwa na Mubarack Amza dakika ya 10 kwa penalti na dakika ya 65.

Azam FC yenye Prince Dube ilishinda bao 1-0 dhidi ya Singida Big Stars yenye Pascal Wawa kwa bao la Sospeter Bajana dakika ya 45.

Previous articleCHAMA MGUU WAKE WA KULIA NI SHIDA TUPU
Next articleIHEFU KIBARUANI TENA LIGI KUU BARA