Home Sports IHEFU KIBARUANI TENA LIGI KUU BARA

IHEFU KIBARUANI TENA LIGI KUU BARA

JUMA Mwambusi, Kocha Mkuu wa Ihefu amesema kuwa makosa ambayo wameyafanya kwenye mechi zao zilizopita watafanyia kazi ili kupata matokeo mazuri.

Ihefu haijaanza kwa kufanya vizuri kwenye mechi za mwanzo ndani ya msimu wa 2022/23.

Ikiwa imecheza mechi 4 haijakusanya pointi zaidi ya kuishia kupoteza mechi zote nne ikiwa nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi.

Mchezo wao uliopita walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya KMC, Uwanja wa Uhuru na ulikuwa ni wa kwanza kwake kukaa kwenye benchi huku Zuber Katwila ambaye alikuwa kocha mkuu akiwa ni msaidizi ndani ya Ihefu.

Leo Oktoba 4 inatarajiwa kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons ambayo imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Sokoine.

Mwambusi amesema:”Tunatambua kwamba matokeo ambayo tunayapata ni mabaya hivyo tunajitahidi kupunguza na kufanyia kazi makosa ambayo tumefanya ili kupata matokeo kwenye mechi zijazo,”.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.

Previous articleMABAO SITA YAKUSANYWA KWENYE MECHI TATU
Next articleHIZI HAPA KUCHEZA LEO LIGI KUU BARA