Home International DE BRUYNE NI NOMA LIGI KUU ENGLAND

DE BRUYNE NI NOMA LIGI KUU ENGLAND

STAA wa Manchester City, Kevin de Bryune anaweza kuingia kwenye vitabu vya rekodi ya Premier.

Sababu kubwa itakayomfanya nyota huyo kuingia kwenye rekodi hiyo ni kutokana na kuanza kwa kasi msimu huu ndani ya kikosi hicho cha Pep Guardiola ambaye ni Kocha Mkuu.

Nyota huyo amekuwa hapo kwa muda mrefu na akiwa ni chachu ya mafanikio kwenye timu hiyo iayotetea ubingwa.

Raia huyo wa Ubelgiji amekuwa ndani ya Etihad kwa miaka saba na kuwa na mabadiliko makubwa ya ukuaji wa kiwango kwa kila msimu.

Msimu uliopita wa 2021/22 alitupia mabao 15 kwenye mechi 30 na alitengeneza pasi nane.

Msimu wa 2021/22 aliweza kufunga mabao sita na kutoa pasi 12 za mabao hivyo bado kasi yake inazidi kupanda kila msimu.

Ikumbukwe kwamba msimu wake bora ulikuwa ni 2019/20 alipoweza kutengeneza pasi 20 za mabao na jumla ana pasi 92 za mabao sawa na nyota wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrad.

Previous articleVIDEO:MANDONGA MTU KAZI AMVAA MWAKINYO
Next articleSAUTI:SABABU NNE ZA MZUNGU WA SIMBA KUTIMKA JUMLAJUMLA