Home International TUCHEL AFUTWA KAZI CHELSEA

TUCHEL AFUTWA KAZI CHELSEA

Thomas Tuchel amefukuzwa kazi ndani ya kikosi cha Chelsea na mmiliki wa timu hiyo ikiwa ni miezi mitatu imepita baada ya kuchukua umiliki wa timu hiyo.

Ni muda mfupi baada ya timu hiyo kupoteza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dinamo Zagreb, ikiwa ni mechi 100 kaweza kukaa kwenye benchi akiwa ndani ya Chelsea.

Inaelezwa kuwa Tuchel alipewa taarifa mapema kuhusu kuondolewa kwake ndani ya Chelsea na Anthony Barry alikuwa anataka akae kwa muda ndani ya timu hiyo mpaka pale mrithi wake atakapopatikana.

Graham Potter anayeinoa Brighton  anatajwa kuwa mrithi wake ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2022/23.

Previous articleKMC YAIPIGA MKWARA SIMBA
Next articleSIMBA WATOSHANA NGUVU NA KMC